Mwenyezi Mungu ameteremsha hadithi bora zaidi
Mwanafikra Ally Mohammad Ash shurafaa Hammadi
Imetafsiriwa na Moharram Ally.
Waislamu waliamini Uislamu na kusadikisha Kitabu cha Mwenyezi Mungu (Qur’ani Tukufu), ambacho kimejumuisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa watu ili kuingia katika dini ya Mwenyezi Mungu Uislamu, na katiba ya Uislamu ni Qur’an na hakuna chochote kinachoongezwa ndani yake au kupungzwa. Na yakitokea hayo, basi mtu huyo atakuwa ameasi ujumbe wa Mwenyezi Mungu aliouteremsha kwa Mtume wake mtukufu. Na Mwenyezi Mungu amesisitiza katika kitabu chake ambacho muislamu anakiamini, na ni sharti kwa kila mwanaadamu ili Uislamu wake uwe sahihi kwa maneno ya Mwenyezi Mungu:
Mwenyezi Mungu ameteremsha hadithi iliyo bora kabisa.” (Az-Zumar:23).
(Na ni nani mkweli zaidi katika kauli kuliko Mwenyezi Mungu) (An-Nisaa:87)
(Na ni nani mkweli zaidi kwa kauli kuliko Mwenyezi Mungu) (An-Nisaa: 122).
Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu akibatilisha hadithi na maneno yote yaliyosababisha uchochezi wa kuuana baina waislamu, kumwaga damu za watu wasio na hatia, kuwagawanya Waislamu kuwa madhehebu na makundi, vyama, kueneza maneno ya chuki na kuhimiza uchokozi, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu. Anamwambia: ((Hizi ni Ishara za Mwenyezi Mungu, tunakusomea kwa haki, basi ni hadithi gani baada ya Mwenyezi Mungu na Aya zake wanaziamini? ” (Al-Jathiya: 6)
Basi ikiwa hadithi bora ni hadithi ya Mwenyezi Mungu na hadithi ya kweli ni hadithi ya Mwenyezi Mungu na neno la kweli kabisa ni neno la Mwenyezi Mungu na hayo ni maneno ya Mwenyezi Mungu aliyoyafikisha Mtume kwa ulimi wake juu ya Mola wake kwa watu. basi je, ni jambo la kimantiki kwa Mtume kutunga Hadith za utunzi wake mwenyewe wakati alipowaambia watu kwamba neno la Mwenyezi Mungu na aya zake ni hadithi bora kabisa na maneno ya kweli?
Kisha Mwenyezi Mungu anamsemesha Mtume wake kwa namna ya kukanusha , vipi Waislamu wafuate hadithi zisizokuwa hadithi za Mwenyezi Mungu katika aya zake? Katika kauli yake Aliyetakasika:
﴾ Hizi Aya za Mwenyezi Mungu tunakusomea kwa haki; basi hadithi gani watakayo iamini baada ya Mwenyezi Mungu na Aya zake? ﴿ Al-Jathiya (6) ).
Aya zake zinazowalingania kwenye amani, rehema, uhuru na uadilifu, na kuharamisha uchokozi na kuharamisha kumuua mtu na kujiepusha na ibada ya masanamu, iwe ya mawe au ibada ya wanaadamu kupitia mawalii na wengineo wanaoombwa, inaonekana kwamba fikra ya Waislamu itabakia kutokuwa na uwezo wa kujikomboa kutokana na ushawishi wa waliotangulia na visa vya uongo vya watu wa kale.
maadamu ameihama Qur-aan na akawasadikisha wapokezi na mapokezi ambayo yamekuwa ni badala ya Aya, zimewafarakanisha Waislamu na kueneza fitina, ndugu kugombana na kupigana makundi tofauti, na zikamwaga damu ya Waislamu, na nyumba zimeharibiwa na watoto wamekuwa walalahoi, kwa athari ya mapokezi na marejeo ya kibinadamu yanayopingana, na kuchukiana, na kila mmoja wao anatafuta ufahari na madaraka, na wamekuwa makundi ambayo yamewadhulumu wengine kwa kiburi na majigambo, na kila mmoja wao anaamini kwamba wao ni wateule kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ili wawe waja wake wasafi, kundi lililookoka, na wengine, marejeo yao ni Jahannam, kwa sababu walizikataa riwaya na wakajiepusha na kufuata marejeo yao ya udanganyifu ambayo yaliharibu ujumbe wa Uislamu.
Na kuwadanganya Waislamu na kuwaingiza katika njia ya Shetani, na kile walichokiita uwongo na upotoshaji wa Sunnah za unabii, na wakajifanya walinzi wa imani kama walivyofanya (Walinzi wa hekalu, miongoni mwa Wakristo wakereketwa wa –Kanisa- Katoliki ulikuwa mwanzo wao Vita vya Msalaba) kati ya wafuasi na wataendelea kuwa Waislamu waliodanganyika zaidi kwa riwaya wanarudiarudia katika kila zama kama alivyowaelezea Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴾Na wanapo ambiwa: Fuateni aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu; wao husema: Bali tutafuata tuliyo wakuta nayo baba zetu. Je, hata ikiwa baba zao walikuwa hawaelewi kitu, wala hawakuongoka? ﴿ Al-Baqarah (170).
Je! Mwenyezi Mungu aliyetakasika, hakusema, akiwafahamisha watu, kwamba kila zama inabeba dhima yake si vyenginevyo, na si jambo la watu kubeba jukumu la wale waliotangulia, au kufuata fikra na imani zao, au kushikamana na tafsiri zao na kuwatakasa Mafaqihi wao. Kwa hiyo, Waislamu katika kila zama ni lazima watafakari juu ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu ili kujua Mungu anataka nini kwa waja wake, heri na maisha mazuri kwa watu, na kujua ukweli katika makusudio ya Aya na hekima ya Mwenyezi Mungu kutoka kwazo, kwa manufaa ya wanadamu, ambayo yatawalinda na upotofu na kuwaonyesha njia ya haki kutokana na uwongo, kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema:
﴾ Hao ni watu walio kwisha pita. Watapata waliyo yachuma, nanyi mtapata mtakayo yachuma; wala hamtaulizwa nyinyi waliyo kuwa wakiyafanya wao. ﴿ Albaqara:134
Maana ya Aya ni kuwa fikra za zama zilizopita na itikadi za watu wa kale hazilazimishwi kwa kila zama, bali watu wa kila zama ni lazima watafakari aya za Qur’ani na wabaini kile zinachokusudia kutoka kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu na makusudio yake, kwa maslahi ya mwanadamu na manufaa yake duniani na akhera, ili Muislamu arekebishe njia yake na akung’ute mavumbi yaliyopita na athari zake, na kile kilichoachwa kati ya urithi, uliowasababishia Waislamu matatizo na majanga, ili hesabu yao ya Siku ya Kiyama isiwe kama wale waliotangulia karne nyingi zilizopita, kwani watakabiliwa na hali ngumu Siku ya Kiyama ikiwa Waislamu wataendelea kuiacha Qur’ani Tukufu mpaka pale atakapotaka Mwenyezi Mungu.
Kwa bahati mbaya, pamoja na kwamba Waislamu waliisoma Qur-aan, hawakufikia malengo ya Aya zake, ambazo baadhi yake zinadhihirisha kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu na kwa ulimi wa Mtume wake ambaye alisema siku ya Hijja ya maagano; Mwenyezi Mungu amesema:
﴾ Leo walio kufuru wamekata tamaa na Dini yenu; basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi. Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini. ﴿ Almaida:3
Na kauli yake aliyetakasika:
﴾ Na yametimia maneno ya Mola Mlezi wako kwa kweli na uadilifu. Hapana awezaye kuyabadilisha maneno yake. Na Yeye ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua. ﴿ An-aam:115
Na kuongezea katika aya zilizopita, Mwenyezi Mungu amewaamuru waislamu kwa kauli yake:
﴾ Fuateni mliyo teremshiwa kutoka kwa Mola Mlezi wenu, wala msifuate rafiki au walinzi wengine badala yake. Ni machache mnayo yakumbuka. ﴿ Aaraaf:3
Na pamoja na kauli ya Mwenyezi Mungu akiwazungumzisha waislamu kwa kauli yake:
﴾ Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. ﴿ Aal-Imran:103
Waislamu wamepuuzia kumtii Mwenyezi Mungu, hivyo riwaya ziitwazo Hadithi zikawatenganisha, cha kujua ni kwamba Mwenyezi Mungu aliwakumbusha Waislamu kuwa maneno yake ni Hadithi bora na ya kweli kabisa, Mtume, amani iwe juu yake, alizisoma kutoka katika aya za Qur’an kwa watu kwa ulimi wake mkweli mwaminifu baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwafikishia watu maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴾ Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu, na ni uwongofu, na rehema, na bishara kwa Waislamu.﴿ Annahl:89
Sasa je, baada ya hayo, Qur’ani inahitaji riwaya zenye kuongeza ndani yake uwongofu na muongozo kwa heri ya wanadamu wote, au kufuata riwaya baada ya kuainishwa na wadanganyifu kwamba ni riwaya inayolingana na maneno ya Mwenyezi Mungu yanayolingania watu washirikiane katika wema, na si kushirikiana katika uadui na juu ya rehema, uadilifu na ihsani, na yale waliyosimulia wapokezi na mafaqihi ya upotoshaji na kughushi juu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, wale ambao wamethubutu dhidi ya maneno ya Mwenyezi Mungu na Qur’ani yake, wakapotea njia na Shetani akawadanganya na kuwasukumia kwenye njia ya uwongo na kufuata shari, uadui na kuvuka mipaka, na akawapeleka kidogokidogo Waislamu kwenye njia batili inayoongoza kwenye moto wa Jahannamu.
Wakati Qur’ani chimbuko lake ni maneno ya Mwenyezi Mungu aliyoiteremsha kwa Mtume wake katika Aya za Qur’ani Tukufu, ambamo anawalingania watu kufuata kitabu chake na kufuata mwongozo wake, ili wasije wakapotea katika maisha haya wakapata dhiki na tabu, bali Mwenyezi Mungu anawatakia watu maisha mazuri, na kuishi vizuri katika kivuli cha amani na utulivu na usalamua, na kusaidiana katika wema na uchamungu, kwa huruma na uadilifu na ihsani, ili kupatikana usalama wa jamii kwa njia ya mshikamano na kusimama pamoja kuwasaidia masikini, wasafiri na wahitaji, na kuwaonea huruma wanyonge, kuwatetea wanaodhulumiwa, na kuwasaidia wanaohitaji, ili baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu ziwashukie walimwengu, na kufuata amri yake kwa kumtii yeye kwa kauli yake:
﴾Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui.﴿ Almaaida:2
Na kwa kauli yake:
﴾Na utafute, kwa aliyo kupa Mwenyezi Mungu, makaazi ya Akhera. Wala usisahau fungu lako la dunia. Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyo kufanyia wema wewe. Wala usitafute kufanya ufisadi katika ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi mafisadi. ﴿ Qasas: 77
Waislamu wamepotea kati ya riwaya
Ni kwa sababu ya uzushi huu na vitendo vya kughushi kutoka katika utunzi wa riwaya na maneno yaliyonasibishwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa uwongo na kashfa, Waislamu (Ahlul-Sunnah wal Jama`ah) wanapotea katika hadithi Zaidi ya 41, zinazoegemea marejeo yaliyoharibiwa na shauku na kutofahamu makusudio ya ujumbe wa Uislamu na hekima ya aya za Qur’ani kwa manufaa ya mwanadamu hapa duniani na huko Akhera, (vitabu vya Al. -Bukhari, Al-Tirmidhiy, Muslim, Abu Daawuud, Al-Nasa’I, na Ibn Majah), pamoja na vitabu vya mafaqihi, maimamu wa madhehebu ya fikra (Al-Maliki, Al-Shafi’I, Al-Hanbali, na Hanafi) wamekuwa marejeo ya kutegemewa kwa ujumbe wa Uislamu, kwani vitabu na dhana hizi zimeunda –fikra- ambazo nyingi zake zinapingana na makusudio ya rehema, uadilifu, amani, ukarimu, kukataza uchokozi dhidi ya mwanadamu, na uhuru kamili wa watu kuchagua imani zao bila ya shuruti, na kutakasa haki ya kuishi kwa mwanadamu, basi Waislamu wakagawanyika baada ya kufuata hadithi za uwongo na mafundisho ya uzushi, na kila Mwislamu akawa anajifakharisha na madhehebu yake ambayo anayaamini, na anachukua kutoka kwake dini yake.
Basi –madhehebu yake- ndiyo bora kuliko madhehebu mengine, basi silabasi za kidini zikawa nyingi yakagongana marejeo ya Kiislamu kwa migongano yao, na kila mmoja wao anaamini kuwa ndiye bora, licha ya kuwa ujumbe wa Uislamu aliouteremsha Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake, amani iwe juu yake katika Qur’an, Mwenyezi Mungu hakumkalifisha yeyote katika wanadamu kuwa wanasihi kwa watu katika kutekeleza ibada na kuwawajibisha kwa uzembe au kuacha kuzitekeleza na kuwawajibisha Waislamu kwa hilo.
Na marejeo ya riwaya hizo yamesababisha hali ya migogoro ya lahaja na ya ubinafsi ambayo iliharibu umoja wa Waislamu, hivyo wakaendeleza mabishano hayo, na mgogoro ukazuka baina yao katika kupigana na kumwaga damu, na nafsi zikafarakana, na kuzalisha vizuizi vya kisaikolojia kati ya madhehebu na makundi mbalimbali yaliyogombana,na hofu na woga vikachukua nafasi ya usalama, na vita vikachukua nafasi ya amani katika jamii za Kiislamu, na uadui ukatawala badala ya ushirikiano ili kufikia utulivu na kupoteza fursa za kujenga, ujenzi na maendeleo, kwa sababu Waislamu walikuwa wakishughulikiana wao kwa wao kutokana na hitilafu na migogoro.
Basi watu wenye tamaa wakakaza nguvu zao juu ya mali za Waarabu na Waislamu, wakawakoloni kwa miaka mingi, wakayakalia makazi yao, na wakavunja haki zao na heshima zao, kwa sababu walivunja amri ya Mwenyezi Mungu kwao kwa maneno yake, Yeye, na aliyo wafikishia Mtume muaminifu:
﴾Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane.﴿ Aal-Imraan:103
Kwa kitu gani waislamu watafanikiwa kushikamana na Kamba ya Mwenyezi Mungu pale watakapotekeleza amri ya Mwenyezi Mungu kwa kumtii, kwa kauli yake:
﴾Fuateni mliyo teremshiwa kutoka kwa Mola Mlezi wenu, wala msifuate rafiki au walinzi wengine badala yake. Ni machache mnayo yakumbuka. ﴿ A’raaf:3
Na wakatekeleza tahadhari yake kwa kumtii na bidi kwa sababu Mwenyezi Mengu aaliyetakasika ni mjuzi Zaidi way ale yaliyofichwa na kadari pale alipozungumza na Waislamu kwa kauli yake:
﴾Na mt’iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu.﴿ Al-anfaal:46
Kadhalika, Mashia wanapotea katika madhehebu mbalimbali kutokana na riwaya tofauti, na hadithi za kutunga, na marejeo mengi, Wanachukua muda wao mwingi katika riwaya yenye madhara zaidi kuliko faida, yametenganisha wengi zaidi ya kuunganisha na yamehimiza dhulma zaidi kuliko kulingania uadilifu na kupandikiza chuki na ukatili katika nafsi zaidi kuliko kulingania rehema, na makundi mengi kati yao yamejitenga na tauhidi na yakamshirikisha Mwenyezi Mungu katika ibada nyingi za kidini, na wakaaamini katika jamaa wa Mtume, amani iwe juu yake, kwamba wao ni waombezi wao kwa Mwenyezi Mungu, watawaingiza peponi, na Mwenyezi Mungu atawasamehe kwa njia ya usuluhishi wao na Mwenyezi Mungu aliyetakasika.
Basi wakaenda mbali na ujumbe wa Uislamu na Masunni na umma na makundi mbalimbali ya Kishia yakawa makundi yanayopigana pale walipoiacha Qur’ani Tukufu na kuwafuata wanachuoni wao na mashekhe wa kidini waliotakaswa na wakawanyanyuwa daraja la unabii na heshima.
Na, Qur’ani ilizizingatia riwaya zote zilizoainishwa kuwa ni hadithi zilizotungwa dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, kama ilivyokuja katika kauli yake, Utakasifu ni Wake:
﴾ Sema: Hao wanao mzulia uwongo Mwenyezi Mungu hawatafanikiwa. ﴿ Yunus:69
Na Qur’ani ilibatilisha kabisa kwa majina yake yote na uainishaji wake, kama ilivyokuja katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu, akimwambia Mtume wake, amani iwe juu yake kwa sura ya kukanusha:
﴾ Hizi Aya za Mwenyezi Mungu tunakusomea kwa haki; basi hadithi gani watakayo iamini baada ya Mwenyezi Mungu na Aya zake? ﴿ Al-Jathiya: 6.
Kadhalika, Ahli Sunnah na Jamaa badala ya kuegemea marejeo ya Qur-aan na sheria ya Mwenyezi Mungu, uwameegemea juu ya madhehebu mbalimbali juu ya vyanzo vya riwaya nyingi zinazopingana na aya za Qur’ani Tukufu,
Ukiongeza pamoja na Mashia na wingi wa madhehebu yao tofauti, na utegemeaji wao wa riwaya maalum kwa kila madhehebu, hivyo wakajianzisha marejeo maalum kama vyanzo pia vya riwaya na hadithi za uzushi ambazo hazikubaliani na vyanzo vya Sunni na Jamaa, na miongoni mwake ni:
“Kitab Al-Kafi” cha Sheikh Abi Jaafar Al-Kulaini kina zaidi ya Hadith 16,199.
Kitabu cha “Man Yahdarih al-Faqih” cha Abi Jaafar bin Muhammad al-Qummi, na kitabu chake kina hadithi “5998”.
Kitabu cha “Tahdheeb al-Ahkam” cha Abu Jaafar Muhammad al-Tusi, ambacho kina hadith “13590”.
Kitabu cha “Istibsaar fiima khtulifa fiihi minal Akhbaar” cha Abu Jaafar Muhammad al-Tusi.
Kitabu cha “Al-Wafi” cha Sheikh Muhammad Murtada Al-Kashani, ambacho kina Hadith “50,000”.
Kitabu cha “Tafseel Wasa’il al-Shia” cha Sheikh Muhammad ibn al-Hasan al-Hurr al-Amili, ambacho kina hadithi “35,850”.
Kitabu cha “Mustadrak al-Wasa’il” cha Sheikh Mirza Husayn al-Tabarsi al-Nuri, ambacho kinajumuisha hadithi “23,000”.
Inaonekana kwamba makundi yote mawili – Sunni na Shia wanategemea hadith kwa mujibu wa mlolongo wa upokezaji wa binadamu, ambao haujaegemezwa kwenye ukumbusho wa hekima kwa mujibu wa chanzo na kutaja kuwa ni marejeo ya msingi ya ujumbe wa Uislamu, kama anavyobainisha msomaji katika mgawanyo wa hadithi kwa watu wa Ahli sunna wal jamaa kama ilivyotajwa hapo awali.
Wakati riwaya hizi zote, hadithi na maneno ya pande zote mbili yanapowekwa mbele ya hukumu ya Qur-aan, hukumu zake zinazingatiwa kwa kulinganisha na Aya, uwepo wake na kutokuwepo kwake na ubatili ni sawa.
Watu huthubutu vipi kufuata riwaya zinazoitwa “hadithi” ambazo ziliandikwa zaidi ya karne mbili zilizopita na watu wasiojulikana itikadi, utambulisho wao, na malengo zilizonasibishwa na Maswahaba wa Mtukufu Mtume; Wanaziamini, na wanazisadikisha, na wanazitakasa, na wanaziacha Aya za Mwenyezi Mungu alizomteremshia Mtume wake muaminifu kwa haki na kuzihama sheria na mawaidha yake, na Yeye anawalingania kwenye njia za wema na amani ili kuwatoa katika giza kuwapeleka katika nuru, anawapatia usalama na utulivu, anawaonyesha yale yatakayowanufaisha, na kuwaangazia njia iliyonyooka, kama ilivyoelezwa katika maneno ya Mwenyezi Mungu, Utukufu ni Wake:
﴾ Mwenyezi Mungu ameteremsha hadithi nzuri kabisa, Kitabu chenye kufanana na kukaririwa; husisimua kwacho ngozi za wenye kumkhofu Mola wao Mlezi. Kisha ngozi zao na nyoyo zao hulainika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Huo ndio uwongofu wa Mwenyezi Mungu, na kwa huo humwongoa amtakaye. Na ambaye ameachwa na Mwenyezi Mungu kupotea, basi hapana wa kumwongoa. ﴿ Huud:23
﴾ Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! ﴿ AlMursalaat:49
Na Mwenyezi Mungu aliyetakasika, anasema tena akisisitiza kuwa maneno yake ndio hadithi na hakuna hadithi nyingine:
﴾ Na ni nani msema kweli kuliko Mwenyezi Mungu? ﴿ Annisaa:87
Na amesema aliyetakasika:
﴾ Huenda ukajihiliki nafsi yako kwa ajili yao, kuwasikitikia kwa kuwa hawayaamini mazungumzo haya! ﴿ Kahf:6
Na Mwenyezi Mungu pia amesema:
﴾ Basi nawalete masimulizi kama haya ikiwa wao wanasema kweli. ﴿ Attuur:34
Mwenyezi Mungu, Utukufu ni wake, kwa Aya zake katika Qur’ani Tukufu, anawapa changamoto wale wote wanaotunga hadithi na kuzihubiri kwa watu, kwamba hizo –aya zake- ndizo njia ya wokovu na ujira kwa wenye kuzifuata na wenye kuziamini ni bustani za neema, kama ilivyokuja katika Aya zilizotajwa hapo juu.
Basi, Mwenyezi Mungu, Utukufu ni Wake, anawapa changamoto waandishi wa riwaya na wazushi wa israiliyaati na maneno ya uongo na waje na hadithi inayofanana na Aya na maneno ya Mwenyezi Mungu katika Qur’ani yake iliyo wazi.
Na mawazo yao yalipopooza, na akili zao zikavurugika, na wakashindwa kupata kile ambacho Muumba wao amewapa changamoto. Walielekeza yale waliyoyataka wao wenyewe kutunga hadithi za uwongo juu ya Mtume na maneno ya uwongo ya ujumbe wa Uislamu, wakikusudia kumzulia Mtume, amani iwe juu yake, katika kuwalingania kwake watu kwenye njia ya wema, usalama, amani na maisha mema duniani, ili wafuasi wa Uislamu wapungue, na walioingia katika Uislamu warudi nyuma kutoka kwenye ahadi yao na Mwenyezi Mungu na Mtume wake na waiache Qur’ani mpaka kuzidhibitiwa akili zao kwa riwaya, uongo na uzushi.
Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaonya wanao mzulia Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa kusema:
﴾ Ni maneno haya ndiyo nyinyi mnayapuuza? ﴿ Waakia:81
Msimamo wa kukanusha umerudiwa katika kauli Yake, Utakasifu ni Wake:
﴾ Je! Mnayastaajabia maneno haya? ﴿ Annajm:59
Kisha anawatahadharisha kwa kauli yake:
﴾ Basi niache na wanao kadhibisha maneno haya! Tutawavutia kidogo kidogo kwa mahali wasipo pajua. ﴿ Alkalam:44
Na aya hizo zilizotajwa zina maana ya uthibitisho wa yale yaliyosisitizwa hapo awali na amri madhubuti ya Mwenyezi Mungu ya kutofuata hadithi zote zinazoitwa hadithi zilizokuja na hadithi za uwongo zilizotungwa dhidi ya Mtukufu Mtume, kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu hakumkabidhi Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, kitu kisichokuwa yale aliyoteremshiwa na Mwenyezi Mungu katika Qur-aan iliyo wazi ili kuzifikisha Aya zake kwa watu wote, Mwenyezi Mungu hakumkalifisha chochote isipokuwa kuwasomea watu Aya zake, kubainisha hekima ya sheria, kuwafahamisha watu makusudio ya kheri na yatakayowanufaisha katika maisha ya dunia na Akhera kutokana na aya zake, na kuwafunza taratibu za ibada kama vile swala, saumu, zaka, kuhiji Nyumba ya Mwenyezi Mungu, na kushikamana na adabu za Qur’an na maadili yake, ambayo yaliunda shakhsia ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na akayatumia katika tabia yake pamoja na familia yake na watu wake na jamii yake katika mazungumzo ya Mwenyezi Mungu Mtume wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kauli yake:
﴾ Basi wewe yashike yaliyo funuliwa kwako. Hakika wewe uko kwenye Njia Iliyo Nyooka. ﴿ Zukhruf:43
Mwenyezi Mungu anamuelezea Mtume wake kazi yake katika kushikamana na kitabu chake katika kuwakumbusha watu Qur-aan na kuwafahamisha Aya zake, na kuwabainishia sheria yake na utaratibu wake ili wapate kuishi katika maisha ya dunia maisha mema kwa usalama na Amani, akithibitisha, Utukufu ni Wake, marejeo ya Qur’an kwa ujumbe wa Uislamu katika amri yake kwa Mtume wake muaminifu:
﴾Basi mkumbushe kwa Qur’ani anaye liogopa onyo.﴿ Qaaf:45
Kama Mwenyezi Mungu anavyomkumbusha Mtume wake kazi ya Mwenyezi Mungu katika kauli yake aliyetakasika:
﴾Ewe Mtume! Fikisha uliyo teremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Na ikiwa hukufanya hayo basi hukufikisha ujumbe wake﴿ Almaaida:67
Ujumbe wa Mwenyezi Mungu, ambao umejumuishwa katika aya za Qur’ani Tukufu, hufikishwa kwa watu na ujumbe mtukufu ambao Muhammad, amani iwe juu yake, anaufanya kwa kueleza malengo ya aya na kubainisha makusudio yake kwa ajili ya kheri ya mwanadamu hapa duniani na akhera.
Aya za Qur’an hazitakiwi kutiliwa shaka na upotoshaji
Katika kipindi cha karne kumi na nne, wapangaji njama hawajaweza kubadilisha au kuongeza kwenye aya za Qur’ani, au kuziweka chini ya hukumu ya akili katika suala la kuaminika, au kuonyesha udhaifu ndani yake katika lengo, maana na muundo, kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwapa changamoto watu kwa kusema:
﴾Na ikiwa mna shaka kwa hayo tuliyo mteremshia mja wetu basi leteni sura moja ya mfano wake, na muwaite mashahidi wenu badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa mnasema kweli. ﴿ Bakara:23
Kama alivyoaihidi kuihifadhi katika kauli yake:
﴾Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda. ﴿ Hijr:9
Aya zake hazitakuwa na mashaka na dhana, hata wahalifu wajitahidi vipi, na maadui wa Uislamu hawatafanikiwa katika majaribio yao ya kughushi na kukashifu Aya zake na mwito wake kwa wema wa wanadamu ili kuwatoa katika giza na kuwaingiza katika nuru, na Mwenyezi Mungu anawapa changamoto kwa kusema:
﴾ Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia. ﴿ Tauba:32
Ama zile riwaya walizoziita Hadith ni misemo ya kibinaadamu, Hadithi za israiliyaati, na maneno ya uongo yaliyosimuliwa, ambazo zimesingiziwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, zikilenga Waislamu kuiacha Qur-aan, na dalili ya kuwa ni uzushi ni pale Hadithi hizo husambazwa kwa aina zaidi ya “41” zinazotungwa na mashetani wa kibinadamu, wamezitengeneza, wakazigawanya, na kuainishwa na watu wenye imani dhaifu, walizieneza na kuziuza kwa watu nguvu za uovu zilizofichika zenye lengo la kuidhoofisha Qur-aan na kuitenganisha na Waislamu, ili kupotea katikati ya riwaya, ambapo Mtume, amani iwe juu yake, anamshtakia Mola wake Mlezi kwa maneno ya Mwenyezi Mungu Mwenyezi:
﴾ Na Mtume alikuwa akisema: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wameifanya hii Qur’ani ni kihame. ﴿ Furqaan:30
Njama dhidi ya Uislamu zikafaulu, na wakapotosha msimamo wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye alikabidhiwa na Mwenyezi Mungu kuwafikishia watu Aya zake na kueleza malengo yake kwa ajili ya furaha na kheri yao hapa duniani, na kuwalipa kwa yale wanayoyafanya kati ya matendo mema kwa kumtii Mwenyezi Mungu, kufuata Kitabu Chake, kutekeleza sheria zake, na kufuata njia Yake kwa maadili mema na tabia njema, kwa rehema, uadilifu, ukarimu, na ushirikiano ili kufikia usalama na utulivu katika jamii za kibinadamu katika sehemu zote, wakamtuhumu Mtume kuwa anapinga kauli zake katika yale anayowafikishia watu kwa njia inayopingana na mazungumzo ya amri ya Mwenyezi Mungu, na wanajaribu kudhoofisha ukweli wake, kwa hivyo wanamsingizia kwa kutunga riwaya ili kushindana na Aya, na wakaunda hali ya ukungu baina ya watu, ya kuchanganyikiwa na shaka baina ya Aya zilizo wazi walizosomewa na Mtume wa Mwenyezi Mungu, na baina ya riwaya zinazopingana na Aya za Ukumbusho wa hikima, wakazua mkanganyiko wa hatari katika imani na akili za watu, ambazo waliziamini wafuasi wa riwaya zilizotajwa kwa misamiati tofauti kwa Hadithi, na nafsi zao gonjwa zilizikubali katika ibada zao kwa sababu ya wepesi wa kuafikiana na nafsi ya mwanadamu, na kutosheleza silika yake bila juhudi katika kupambana na nafsi, kuzuia matamanio yake na kuiongoza, na kuichochea kwenye upotofu na dhambi, basi Mwenyezi Mungu atawasamehe kwa maneno ya kunena kwa ndimi tu, kama walivyo wahadaa Waislamu kwa riwaya hizo za kutunga zinazopingana na Aya za Kitabu kilicho wazi, hazikubaliani na mantiki na masharti ya Waumini ambao Mungu atawaingiza Peponi.
Inaonyesha uwongo wa wale wanaopenyeza jina la Uislamu ili kutekeleza malengo yao maovu ya kupotosha sifa ya Mtume na kudhoofisha hadhi yake, kama mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu hadi kwa watu wote, anazungumza nao kwa akili na anawalingania watu juu ya dini ya Mwenyezi Mungu kwa uhuru wote ili waweze kupambanua baina ya haki na batili kwa kufuata anayowaongoza kwenye njia ya amali njema na uwongofu, na analeta usalama, utulivu, na amani kwa watu katika maisha ya dunia, huku akiwafikishia watu Aya za Qur’ani zenye hekima kwa wito wake.
Wamewakinaisha watu kwamba mwenye kufuata riwaya na juhudi na kazi wanayompunguzia mwanadamu na suhula wanazozitoa katika kushikamana na sheria na njia ya Mwenyezi Mungu na kutoshikamana na aya za Qur’ani Tukufu zinazowalingania kumwinua mwanadamu katika imani, maadili na haki, wanachuoni wa Hadithi, mafaqihi na wafasiri wamewahadaa Waislamu kwa kuwatosheleza na maneno fulani ambayo ndimi zao hutamka bila ya kuswali swala ya faradhi, kwa kutumia sharia ya Mwenyezi Mungu na kufuata njia ya Mwenyezi Mungu.
Maimamu wa Uislamu na masheikh wa dini watadhamini kwao malipo makubwa na wataingia kwenye mabustani ya neema bila ya kutekeleza faradhi kama alivyoamrisha Mwenyezi Mungu, na yanayotakiwa miongoni mwa ikhlasi na uaminifu kwa Mwenyezi Mungu, na utekelezaji wa ahadi ya mwanadamu kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Kutokana na kujitahidi kwa nafsi na kuilazimisha kushikamana kikamilifu na matumizi ya sheria na njia yake, na wamerahisisha kufuata riwaya zinazotimiza ndoto zao za upotofu, kwa kuingia Peponi, kama baadhi ya riwaya wanazozihusisha na Mtume, amani iwe juu yake, kwa kauli yake:
(Atakaye niswalia mara elfu kwa siku hatakufa mpaka abashiriwe Pepo.)
Kwa sababu kusema kwa ulimi ni rahisi zaidi kwa mtu kuliko kupigana na nafsi na shetani, na kulazimiana na ujumbe wa Uislamu ndani ya Qur’ani Tukufu na yale yanayomtaka Muislamu kushikamana na sharia za Mwenyezi Mungu na kutumia njia ya Mwenyezi Mungu, na kinachohitajika miongoni mwa kupigana na nafsi na kudhibiti silika yake, Kwa hiyo, kutamka kwa ulimi ni rahisi zaidi kwa mtu kumswalia Mtume mara elfu, maadamu malipo ya Pepo yamedhaminika.
Hivyo ni kawaida kwamba yaliyomo ndani ya riwaya yameelekea zaidi kwenye nafsi na kumpunguzia Mwislamu mizigo yoyote inayohitaji kuhangaika na nafsi, ili kufahamu masharti ya kubeba dhima ya ujumbe wa Kiislamu katika kushikamana na sheria za Mwenyezi Mungu na kuitumia njia ya Mwenyezi Mungu katika maisha na muamala katika maisha haya ya dunia.
Lakini balaa atakalokumbana nalo mtu Siku ya Kiyama, pale atakapomsikia anayezungumza naye ni wema gani umefanya katika maisha yako, na mtu huyo akajibu kwa majuto:
﴾ Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo, siku hiyo mtu atakumbuka! Lakini kukumbuka huko kutamfaa nini? ﴿ Alfajr:23
Jambo hilo likawachanganya watu, kwani riwaya za uzushi dhidi ya Mtume ziliwasababishia, kati ya kitendo na kauli, kwani sunnah ya Mtume (s.a.w.w.) ni sifa zote za wema ambazo zimetajwa ndani ya Qur’ani Tukufu na maadili tukufu ambayo Mwenyezi Mungu alimtaka ziwe mwenendo wa maisha yake baina ya watu, katika kuamiliana kwake nao na mahusiano yake nao, na kuwalingania kwa hekima na mawaidha mazuri ya kuingia katika Uislamu, kwa sababu Sunna ni matumizi ya kivitendo katika kila kitu kilichotajwa katika Sheria za Qur’ani Tukufu, mielekeo ya kimaadili, na muamala mzuri kwa sheria ya Mwenyezi Mungu, ili Waislamu waweze kufuata mfano huo wa Mtume muaminifu na wafuate anayowaonyesha, matendo mema na kuwahadharisha na njia ya uwongo, kwa kuwajali watu wasiingie kwenye makucha ya Shetani na vishawishi vyake ambavyo vitawatia hasara katika maisha ya dunia na Siku ya hesabu, kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
﴾ Hakika nyinyi mnayo kiigo chema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu﴿ Al-Ahzab: 21
Kiigo ni mwenendo na muamala mzuri, kwa kutekeleza adabu za Qur’an, na Sunnah ya kweli na halisi ni kiigo, na kiigo ni kazi.
Mwenyezi Mungu anataka waja wake waige tabia ya Mtume katika maadili na muamala wake na watu wote, bila ya ubaguzi (kwa rehema, uadilifu, ukarimu, amani, na kuheshimu haki za binadamu katika imani yake, na kuheshimu haki yake ya kuchagua kwa hiari dini aitakayo, kuhifadhi haki yake tukufu ya kuishi, na kujitolea kutoifanyia uadui, kwa njia zote, na maadili mengine ya juu yaliyotajwa katika Aya za Qur’ani Tukufu.
Na kwa sababu ya upotoshaji wa Sunnah halisi, na kutumia jina la “Sunnah” katika riwaya zilizozushwa dhidi ya Mtume, jambo hili limesababisha maafa kwa Waislamu, ikiwa ni pamoja na kugawanyika, mifarakano, na mapigano kutokana na kukithiri kwa marejeo, na bughdha na chuki imeenea kati yao badala ya mapenzi na kuhurumiana na ushirikiano, kama alivyoamuru Mwenyezi Mungu, akisema:
﴾ Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui.﴿ Maida:2
Misiba na maafa hayo yaliyotokana na madai ya riwaya dhidi ya Mtume, kwa dhulma na uzushi, yalitokea zamani, na yaliyotokea yanaendelea hadi leo, vizazi vya Kiislamu vinapitisha sumu na uwongo huo juu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, na damu inaendelea. kumwagwa, watoto kuhamishwa, na wanawake kuongozwa kama watumwa kwenye soko la utumwa na starehe.
Wamenyimwa ubinadamu wao, na kuongozwa mpaka kwenye kufa kwao, kuuawa bila haki, na kuvalishwa mikanda ya kulipuka pamoja na watoto, kuwaua watu wasio na hatia na wao wenyewe.
Haya ni matokeo ya yale ambayo baadhi ya mashekhe wa kidini waliyapandikiza mawazo potofu, ya kihalifu yanayotokana na simulizi za kishetani katika fikra za Waislamu, hivyo wakawapoteza na kuwaingiza katika matendo ambayo Mwenyezi Mungu amekataza watu kuyafanya. Ili wawe kuni katika moto wa Jahanamu.
Damu kiasi gani zilimwagika?
Ni miji mingapi iliharibiwa?
Ni wanawake wangapi wamekuwa wajane kwa sababu ya riwaya hizi, na kile walichokiita kuwa ni sunna tukufu?
Leo, jinai hizi zinatokea kwa jina la Uislamu, kutoka kwa ISIS, Takfiri, Udugu, Al-Qaeda, na wengine wanaonyanyua kauli mbiu ya Uislamu kwa jina la Mungu ni Mkuu, wanaua watu wasio na hatia, wanaharibu miji na kuwahamisha watoto.
Je, hivi ndivyo Waislamu wanataka kupotosha sura ya dini ya Kiislamu na kudhuru hadhi ya Mtume, rehema na amani ziwe juu yake? Na kupotosha wasifu wake wenye harufu nzuri? Na kupotosha sura ya ujumbe wa Uislamu, unaotaka rehema, ihsani na uadilifu?
Lau wangefuata yale aliyowaamrisha Mwenyezi Mungu watu katika Kitabu kilicho wazi na maisha ya Mtume, matendo yake na tabia yake, basi maafa haya yasingewapata Waislamu tangu karne kumi na nne zilizopita mpaka leo, lakini Waislamu wengi bado wanasisitiza kwamba simulizi za uwongo, israiliyaati, na hadithi zinazonasibishwa kwa Mtume ni Sunna ya Mtume ambayo ni lazima ifuatwe na ndiyo marejeo ya kisheria kwa Waislamu.
Mbali na hayo, Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitajwa kuwa ni Qur’ani inayotembea, inayosisitiza matumizi yake ya sifa zote tukufu na mambo ya wema katika mwenendo wake na muamala wake na watu, na kwa ajili hiyo Mwenyezi Mungu Mwenyezi Amemuelezea:
﴾ Na hakika wewe una tabia tukufu. ﴿ Al-Qalam: 4
﴾ Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote. ﴿ Anbiyaa:107
Je, mtu mwenye sifa hizi atawataka watu wawaue watu wasio na hatia, wawashambulie, kuwatenga wale wasiokubaliana na dini yake, kukataa kurudisha amani kwa wale wanaoamini dini nyingine, kushambulia haki za watu, kuzungumza juu yao wakati hawapo, au kukamata haki zao?
Sifa hizi alizozieleza Mwenyezi Mungu kwa tabia ya Mtume wake zinatofautisha baina ya Muumini wa Kiislamu na Muislamu ambaye anajali mambo ya ibada tu na hivyo anakuwa Mwislamu kwa jina na akapuuza kumfuata Mtume katika maadili na muamala wake. akisema:
(Na ni nani mbora wa kauli kuliko yule anayelingania kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na akasema: “Hakika mimi ni katika Waislamu.) Fassilat : 33».
Msemo huo umehusishwa na matendo mema, kama ilivyoelezwa ndani ya Qur’ani Tukufu, kwamba ina maana ya kufanya ibada za faradhi katika nyakati zake zilizowekwa, kufikia malengo yake kwa mujibu wa matakwa ya Mwenyezi Mungu, kwa kutumia sheria za Mwenyezi Mungu, kuzingatia maadili ya kibinadamu, mahusiano, kazi, na kuchukua rehema kama kanuni katika mahusiano ya kibinadamu na uadilifu, kanuni ya milele, na maadili katika tabia na ya miamala kati ya watu, na kufanya matendo ya ibada, na yale yanayohitajika, kuzifanya kwa nyakati zilizowekwa, kama vile Swala, Saumu, Zaka, na Hijja kwenye Nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu, Mwislamu sio tu anayeswali na kuhiji na kutoa zaka, bali ni mtu anayejitahidi kufikia malengo yake, kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema katika Qur’ani Tukufu:
(Hakika Sala inakataza machafu na maovu.) Al-Ankabut: 4 5 »
Hili ndilo lengo kuu la kuswali, basi, Iwapo swala haimtoharishi mtu baada ya kuswali, basi swala yake haina thamani, kwa sababu haikufikia lengo lake la kujiepusha na mambo machafu na maovu.
Swala si harakati za kiriadha tu, bali ni uthibitisho kutoka kwa mwenye kuswali kwamba yumo katika agano lake na Mungu kwamba maombi yake yatamzuilia mambo machafu na maovu, na yote yanayomkasirisha Mwenyezi Mungu, awe yuko na Mungu au katika maeneo yake na watu, kwani Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema kuhusu zakat:
(Wale wanaotoa mali zao katika njia ya Mwenyezi Mungu kisha hawafuti walicho toa kwa masimango wala maudhi, Malipo yao yako kwa Mola wao Mlezi, wala hawatakuwa na khofu juu yao, wala hawatahuzunika) Al-Baqarah – 262»
Hivyo, Mwenye kutekeleza faradhi ya zaka, na mpaka Mwenyezi Mungu aikubali kutoka kwake na amlipe thawabu ya kuitekeleza kutokana na mambo ya kheri, asijigambe kwayo kwa watu, wala asiwadhuru kwa kauli au vitendo, kama vile Mwenyezi Mungu Mtukufu anavyowaonya watetezi wa Uislamu. , Mashekhe wa Dini na Mafakihi dhidi ya kuficha watu kuhusu hakika ya malengo na makusudio ya Aya za heri na wema kwa mwanadamu na wanayoyaficha kuhusu anayotaka Mwenyezi Mungu katika Aya na wanawahadaa Waislamu kutokana na maelekezo ya Mwenyezi Mungu katika ukumbusho wenye hekima unaowaletea manufaa watu katika maisha ya dunia na kuwapatia radhi za Mwenyezi Mungu, ili awalipe Akhera mabustani yenye neema, anawatahadharisha Mwenyezi Mungu waislamu kutoficha alichomteremshia mtume muaminifu miongoni mwa uwongofu na uwazi, kwa kauli yake:
“Hakika wale wanaoficha hoja na uwongofu tulizoziteremsha baada ya kuzibainisha kwa watu katika Kitabu, hao amewalaani Mwenyezi Mungu, na wanawalaani walaani” Al-Baqarah: 159.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Akasema katika onyo jengine, kwa wale wanaoficha aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu:
(Hakika wale wanaoficha aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu katika Kitabu na wakakibadilisha kwa thamani ndogo, hao hawana wanachokula matumboni Mwao isipokuwa moto, na Mwenyezi Mungu hatasema nao Siku ya Kiyama, wala hatawatakasa, na watapata adhabu chungu.” (Al-Baqarah – 174).
Hivyo, Waislamu wasiamini riwaya zote zilizonasibishwa kwa Mtume na zilizozushwa, kama vile israiliyati na maneno ya uzushi, watabeba mzigo wa yale waliyomsingizia Mwenyezi Mungu na Mtume Wake Siku ya Kiyama, mzigo kwa yule aliyesambaza na kuyatangaza na kuyaeneza, au kuziamini hadithi hizo, na hatima yake itakuwa ni laana ya Mwenyezi Mungu na atatupwa Motoni na atakabiliana na adhabu kali Siku ya Kiyama kwa kauli yake:
(Sema: Hakika wale wanaomzulia Mwenyezi Mungu uwongo hawatafanikiwa.) Yunus: 69.
Kwa hiyo, Waislamu lazima waige Sunna ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambayo imetajwa katika Aya nyingi za Qur’ani Tukufu, kwa kumtii Mungu katika kutekeleza sheria na njia yake, kama Mwenyezi Mungu alivyosema:
(Hakika mna mfano mwema kwenu kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu mara kwa mara) Al-Ahzab: 21.
Na Mwenyezi Mungu amemuelezea Mtume wake kwa kusema:
(Hakika amekujieni Mtume kutoka miongoni mwenu, na yale mliyopata ni mazito juu yake, anakuhangaikieni Waumini, Mwingi wa upole na Mwenye kuonea huruma)
Surat Al-Tawbah: 1) 28».
Kama vile Mwenyezi Mungu alivyozungumza na Mtume wake kwa kuwalingania Waislamu kumpenda Mwenyezi Mungu kwa kufuata yale aliyowafikishia Mtume Wake mwaminifu kuhusu Aya za Ukumbusho wenye hekima, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:
(Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyezi Mungu, basi nifuateni mimi, Mwenyezi Mungu atakupendeni na atakughufirieni madhambi yenu Kwani Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.) Al Imran: 31.
Basi Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anawatakia watu wote wawe wameridhiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu na awapende ili awaghufirie madhambi yao na awarehemu duniani na akhera, na awaonyeshe Mtume njia iliyonyooka ili Mwenyezi Mungu awapende kwa kumfuata Mtume wake kuwa ni kigezo na mfano wenye kutumia sheria ya Mwenyezi Mungu katika maisha yake na muamala wake na jamaa zake na watu wake na watu wote wenye tabia za Waumini wa kweli walioelezwa katika Qur’ani Tukufu, kiibada, kimaadili, na kushughulika na yale yanayompendeza Mwenyezi Mungu, kwa sababu Mtume wa Uislamu, amani iwe juu yake, anawajali waja wa Mwenyezi Mungu.Anawatarajia kheri na uadilifu, anawaonyesha njia za matendo mema, na anawaita katika mabustani ya neema Akhera na Mwenye kushikamana na sheria ya Mwenyezi Mungu katika maisha yake na kufuata kitabu chake, Mwenyezi Mungu atamjaalia kuishi pepo na furaha duniani na kumlipa Pepo ya neema Akhera ya kudumu humo milele.
Na atakaye jiepusha na kukifuata Kitabu chake kilicho wazi, Mwenyezi Mungu atamjaalia maisha yake kuwa dhiki, tabu na Jahannam, kama alivyosema Mwenyezi Mungu:
(Na atakayepuuzia ukumbosho wangu basi atakuwa na maisha ya dhiki, na tutamfufua kipofu Siku ya Kiyama.) Taha-124.
Na Siku ya Kiyama malipo yake ni Jahannam na ni marejeo mabaya.
***