Alarab Language

Bwawa la “Julius Nyerere”… Mfano wa Ushirikiano Imara wa Misri na Nchi za Bonde la Mto Nile  

Na, Ramy Zuhdi, Mtaalam wa Masuala ya Afrika  

Misri inathibitisha, mara kwa mara, kwamba jukumu lake barani Afrika si kauli mbiu wala matukio ya kidiplomasia, bali ni ahadi ya kihistoria na sera imara inayoamini kwamba mishipa ya damu ya bara hili, kama Mto Nile, si vyanzo vya migogoro bali ni vijito vya maisha ya pamoja vinavyoleta maslahi na kuunganisha malengo. Katika moyo wa dira hii, nchi kumi na moja za Bonde la Nile zinzutambua mto huu kama ni kitu muhimu kwa Misri, na ndio nguzo ambayo Cairo inatumia kukuza maendeleo na kuunda ushirikiano wa kweli mbali na hotuba ya kinadharia na mahusiano ya kimfumo.

Sambamba na mwelekeo huu, mradi wa Bwawa la “Julius Nyerere” nchini Tanzania unajitokeza kama mojawapo ya mifano muhimu ya kisasa inayoonyesha dhana ya ushirikiano wa Misri na Afrika katika uhalisia . Mradi huu si tu kituo cha kuzalisha umeme wa maji, bali ni kichwa cha habari cha hatua mpya ya ushirikiano, kikisisitiza tena uwezo wa Misri wa kuleta maendeleo ndani ya bara, na sio tu kuunga mkono kwa uzoefu au ushauri .

Bwawa hili limejengwa kwenye Mto Rufiji  , na linahesabiwa kuwa mojawapo ya mabwawa makubwa zaidi ya kuzalisha umeme wa maji barani Afrika, likiwa na uwezo wa kuzalisha hadi Megawati  2115. Huu ni uwezo wa kutosha kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya nishati nchini Tanzania  , kutoa umeme kwa mamilioni ya wananchi  , na kuwezesha nchi hii rafiki kufikia utulivu wa viwanda, kilimo, na huduma unaohitaji nishati salama na endelevu . Umuhimu wa bwawa hili pia unatokana na ukweli kwamba linawakilisha utii wa msingi katika dira ya Tanzania ya kufikia maendeleo yanayotegemea nishati safi na kupunguza utegemezi wa mafuta au gesi.

Lakini thamani halisi ya mradi huu inavuka hata takwimu na teknolojia . Bwawa hili ni ushahidi mpya wa uwezo wa makampuni ya Misri kutekeleza miradi mikubwa nje ya mipaka yake, baada ya kujikusanyia uzoefu mkubwa nchini Misri katika ujenzi wa mabwawa makubwa na miradi ya miundombinu iliyobadilisha sura ya nchi katika miaka iliyopita . Makampuni ya Misri yalifanikiwa kuhamisha uzoefu huu kwenda Tanzania kwa uwezo wa kivitendo na nidhamu ya kihandisi inayolingana na jina la Misri barani Afrika .

Jukumu la Misri halikuwa jukumu la kampuni ya utekelezaji tu  , bali jukumu la nchi kamili iliyoamua tangu mwanzo kwamba mradi huu uwe mfano wa ushirikiano wa dhati wa Kiafrika . Cairo ilikuwepo kisiasa na kiufundi katika hatua zote za mradi  , kuanzia kuunga mkono makubaliano hadi kurahisisha kazi na kutoa uzoefu  , hadi ufuatiliaji mwendelevu ili kuhakikisha utekelezaji unafanywa kwa viwango vya juu zaidi vya ubora na ufanisi . Jukumu hili linaonyesha dira ya Misri iliyo wazi kwamba kuunga mkono maendeleo barani Afrika si msaada wala mwonekano wa vyombo vya habari, bali ni uwekezaji katika kutafuta utulivu wa eneo hilo, na muendelezo wa asili wa maslahi ya pamoja .

Bwawa hili pia linawakilisha mwendelezo wa mfululizo mrefu wa miradi ambayo Misri imeendelea kuunga mkono katika nchi za Bonde la Nile katika sekta za elimu, afya, kilimo, na umwagiliaji, pamoja na ufadhili wa masomo, programu za mafunzo, na misheni za matibabu . Misri inaona kuwezesha nchi za Afrika kama msingi wa kujenga ushirikiano imara na wa kweli, usiotegemea misaada ya kawaida bali ni ushirikiano wenye uwiano na unaoleta maendeleo endelevu .

Mradi huu pia unajumuishwa na sera ya Misri ya kina zaidi inayohusu usimamizi wa rasilimali za maji, ulinzi wa mazingira, na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi ndani ya Bonde la Nile . Cairo inatambua kwamba Mto huu mkubwa si tu chanzo cha maji  , bali ni msingi wa kujenga mifumo ya kiuchumi inayoweza kuvutia uwekezaji  , kuboresha kiwango cha maisha  , na kuimarisha mawasiliano kati ya watu . Kutokana na msingi huu, Misri daima inapendekeza dira za suluhisho la pamoja kulingana na kanuni za kutodhuru na kufikia maslahi yenye uwiano kwa wote .

Uzoefu wa Bwawa la “Julius Nyerere” unafunua wazi kwamba Misri haitafuti maslahi madogo wala kushughulika na nchi za bonde kwa sera ya kufanya vitu vyapesi tu, bali inachagua njia ngumu zaidi na ya dhati: Kujenga uaminifu wa muda mrefu ambao msingi wake ni mafanikio, maendeleo, na usawa . Hili limeonekana katika msaada endelevu wa Misri kwa makampuni yanayofanya kazi katika mradi huo  na kurahisisha kila kitu muhimu ili kuhakikisha bwawa linakuwa hadithi ya mafanikio ya Kiafrika iliyoandikwa kwa herufi za Misri na Tanzania pamoja .

Leo, huku utekelezaji wa mradi ukikaribia hatua zake za mwisho, ukweli unathibitishwa kwamba Misri ni mshirika anayeaminika  , na kwamba uwezo wake wa kujenga, kutekeleza, na kupanga hautenganishwi na nia yake ya dhati ya kuona Afrika yenye nguvu na utulivu zaidi . Bwawa hili si tu mradi wa nishati safi  , bali ni sehemu ya dira ya Misri inayoona kwamba mustakabali wa bara unajengwa kwa ushirikiano  , na kwamba Mto Nile unapaswa kuwa daraja la kuunganisha sio uwanja wa migogoro  , na unakuwa chanzo cha maendeleo sio chanzo cha mvutano .

Mwishowe, Mto Nile unabaki – kama Misri inavyosisitiza daima – fursa ya maisha inayounganisha na sio kutenganisha, na kuwa utambulisho wa pamoja mkubwa kuliko mipaka ya kisiasa . Kwa ufahamu huu, Misri itaendelea kuunga mkono ndugu zake katika nchi za bonde na kufanya kazi katika kujenga miradi ya maendeleo inayoongeza uwezo wa bara kujitegemea  , kwa sababu Misri inaposonga mbele barani Afrika, inasonga mbele kutokana na ufahamu kwamba mustakabali wake ni sehemu isiyotenganishika ya mustakabali wa bara zima .

اظهر المزيد

موضوعات ذات صلة

زر الذهاب إلى الأعلى